Nafasi ya sekta ya mawasiliano katika kulipeleka taifa letu kwenye uchumi wa kati

0
35

Lengo la Taifa lolote duniani kufikia uchumi wa kati huwa na changamoto nyingi. Takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa nchini Tanzania tunayo bahati kwamba kwa muongo mmoja uliopita tumekuwa na uchumi imara na ukuaji mkubwa wa pato la taifa wa wastani wa asilimia 8. Sambamba na hilo takwimu hizo zinaonyesha pia kuwa Tanzania imehakikisha kuwa ukuaji wa ajira rasmi na zisizo rasmi unabaki katika kiwango kizuri, kikiwa kwenye wastani wa asilimia 1.9.

Mafanikio haya makubwa ya kiuchumi na soko la ajira yamechangiwa kwa kiasi fulani na sekta binafsi na biashara mihimili katika sekta hiyo ikijumuisha teknolojia, ujenzi na mawasiliano. Kwa pamoja makampuni katika maeneo hayo matatu yametoa ajira kwa idadi kubwa ya Watanzania.

Mojawapo ya sababu ya makampuni katika eneo hilo kufanikiwa katika suala la kutoa nafasi za ajira ni kwa sababu huduma zake zinahitajika katika sekta nyingine zote za uchumi.

Kusisitiza hilo, kwa mfano tuitazame sekta ya mawasiliano ya simu. Aina ya ajira ambazo sekta hii inatoa zinakwenda mbali ya namna ambavyo awali ilitazamwa. Mfano sekta hii ina mawakala wa fedha, wasambazaji na wauzaji wa huduma za simu, wataalamu wa huduma kwa wateja na wengineo.

Zaidi ya hiyo, sekta hiyo pia inahitaji wataalamu toka maeneo mengine mengi mfano wahandishi wa mitambo ya mawasiliano na wachambuzi wa takwimu.

Wapo wataalamu lukuki wa fani mbalimbali ambao wanahakikisha masaa 24 mitambo iko sawa kutuwezesha kupata huduma na kutumia simu zetu bila tatizo mfano kuperuzi mtandaoni, kununua bando, kutuma na kupokea pesa, SMS, na nyingine nyingi.

Tigo Tanzania ni mfano mmojawapo wa kampuni hizo. Kampuni hii inatajwa kama mwajiri muhimu nchini ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 115,000 wenye ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Nchi yetu haina budi kuendelea kuunga mkono sekta hii na wadau wake wa namna hiyo ili kusukuma mbali zaidi gurudumu la maendeleo ya uchumi wetu.

Send this to a friend