Nafasi ya teknolojia ya kidijitali katika kuendeleza uchumi wa Tanzania

0
45

Na Martin Nyeka UDBS

Katika miaka mitano iliyopita, idadi ya watumiaji wa simu katika eneo la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara imeongezeka mara dufu. 

Kwa mujibu wa GSMA (Shirika la Kimataifa la Makampuni ya Simu), mpaka mwisho wa mwaka 2018, idadi ya watumiaji wa simu za mkononi katika eneo hili ilikuwa imeongezeka kwa milioni 20, ukilinganisha na mwaka uliotangulia (2017). Makadirio yanaonesha kwamba idadi hiyo itaongezeka kwa watumiaji wapya milioni 167 kufikia mwaka 2025.

Hapa Tanzania, takwimu za siku za karibuni toka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) zinaonesha kwamba kulikuwa na laini za simu milioni 49 mpaka kufikia mwisho mwaka 2019.  Tukitazama mbele, makadirio ya sasa yanatupa ubashiri kwamba kati ya mwaka 2018 hadi 2025 Tanzania itaongeza watumiaji wapya wa simu za mkononi milioni 10.

Ongezeko hili linatokana sana na sekta imara ya mawasiliano ya simu nchini. Pia ni ishara kwamba Watanzania wana ari na nia ya kuendesha maisha yao kidijitali na kuelekea kule dunia inapoelekea katika mapinduzi ya kiteknolojia. Tunaweza basi kusema bila shaka yoyote kwamba uwekezaji katika teknolojia ya kidijitali utakuwa na nafasi kubwa kabisa katika maendeleo ya nchi hizi sasa na katika siku za usoni. Kama alivyonukuliwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, “Dunia ijayo ni ya kidijitali zaidi kuliko dunia iliyopita”.

Kampuni za mawasiliano ya simu Tanzania, zinafanya kila ziwezalo kuhakikisha kwamba wateja wao wako mstari wa mbele kufaidi matunda ya maendeleo ya kidijitali. Mfano huduma ya Tigo Pesa toka kampuni ya Tigo Tanzania imechagiza maendeleo ya mfumo rasmi wa fedha nchini. 

Huduma kama Tigo Pesa imewaleta Watanzania wengi katika mfumo rasmi wa fedha hasa wale waliokuwa wakiishi maeneo ya vijijini. Ubunifu mwingine wa kiteknolojia toka Tigo ni ule wa simu ya Kitochi 4G inayowasaidia watumiaji wake kuendelea kuwasiliana kirahisi kupitia intaneti kwa programu kama barua pepe, Facebook na WhatsApp. 

Jinsi nchi yetu inavyoendelea kushuhudia watumiaji wa simu za mkononi wakiongezeka, ni jambo jema kuona kampuni za simu kama Tigo zikiwa bunifu kunufaisha wateja wake.

Send this to a friend