Nafurahia Musiba kuwatukana viongozi wastaafu (CCM)- Mbunge Livingstone Lusinde

0
15

Mimi nafurahi Cyprian Musiba kutukana viongozi wastaafu, kwa sababu Kinana (akiwa Katibu Mkuu) alitukana viongozi wake akawaita mizigo. Nape (akiwa Mwenezi) amepata umashuhuri kutokana na matusi. Nashangaa wanakasirika nini, wakati wameunda utaratibu huu.

Hayo yamesemwa leo na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alipokuwa akizungumzia mivutano inayoendelea ndani ya chama hicho ambapo amsema kuwa Nape na Kinana hawapaswi kulalamika kuhusu watu kutukanwa kwa sababu wao ndio walioasisi utaratibu huo.

Katika hatua nyingine mbunge huyo amemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwachukulia hatua viongozi hao wastaafu wa CCM kwa kile alichosema haiwezekani watu wakamtukana na kumdharau Rais halafu wakaachwa.

Huwezi ukasema mkuu wa nchi mshamba au kuwa amechanganyikiwa, huo ni ukosefu wa nidhamu uliopitiliza, nina uhakika Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru amesikia na atachukua hatua. Nashangaa Waziri Lugola hajawachukulia hatua. Rais awe mshamba, mjanja awe Nape! Nape nani?

Amesema kuwa wanachama wa CCM wasiwe na hofu kwa sababu hakuna mgogoro wowte ndani ya chama hicho, badala yake kuna mgogoro wa watu binafsi.

Ameongeza kuwa migogoro baina ya watu hao inakuja siku chache baada ya ripoti ya kuhakiki mali za chama kukamilika, hivyo wanatafuta pa kujificha. Amemuomba Rais Dkt Magufuli kuiweka hadharani ripoti hiyo huku akieleza kuwa kuna viongozi waliokwapua mali za chama, na endapo ripoti hiyo itatolewa, hatutawaheshimu tena.

Kuhusu Bernard Membe ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Lusinde amesema atashughulika naye atakaporejea nchini kutoka China anapopaswa kwenda kwa kazi za kibunge.

Amekanusha madai kuwa wabunge wanapangwa kuzungumzia yanayoendelea ndani ya chama hicho tawala, na kwamba yanayofanywa na Musiba waliyaandaa hao leo wanaolalamika, hivyo ni vyema wakatulia.

Send this to a friend