
Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi nchini Kenya, Eliud Lagat amekaa pembeni kupisha uchunguzi juu ya kifo cha mwanablogu Albert Ojwang aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi.
Katika taarifa yake ya Jumatatu, Lagat amesema ameamua kwa hiari na baada ya kufikiria kwa kina kuachia nafasi hiyo kwa muda kwa manufaa ya umma na heshima ya ofisi yake.
Ameongeza kuwa majukumu yake yatatekelezwa na naibu wake hadi uchunguzi unaoendeshwa na Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) utakapokamilika huku akiahidi kutoa ushirikiano na kutoa pole kwa familia ya marehemu.
Kifo cha Ojwang’ kimeibua hisia kubwa nchini Kenya, huku maandamano na wito wa kuwajibika kwa maafisa wa juu wa polisi yakiongezeka.