Naibu Katibu Mkuu CHADEMA akamatwa uwanja wa ndege akielekea Ubelgiji

0
1

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amani Golugwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku wa kuamkia leo akiwa katika maandalizi ya kuelekea Brussels nchini Ubelgiji.

Taarifa iliyotolewa na Polisi imesema Golugwa amekamatwa kufuatia taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa nchini.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa kina wa taarifa hizi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama,” imesema taarifa ya Polisi.

Aidha, limewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizo za kisheria zinazomhusu mtajwa.

Send this to a friend