Naibu Waziri: Hakuna chombo cha habari kilichofungiwa katika kipindi cha Rais Samia

0
44

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amesema katika kipindi cha miaka miwili cha Rais Samia Suluhu Hassan hakuna chombo chochote cha habari kilichofungiwa.

Akizungumza alipokuwa katika maadhimisho ya miaka 30 ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika visiwani Zanzibar, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kukuza uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.

Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaanza kutumika nchini

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) usajili wa vyombo vya habari umeongezeka kutoka kituo kimoja cha redio na magazeti 10 baada ya uhuru wa Tanganyika hadi kuwa na magazeti 312, redio 218, televisheni 68, redio za kimtandao 8, televisheni za mtandao 391, blog na majukwaa 73 na ‘cable operators’ 53 waliosajiliwa.

Aidha, amebainisha kuwa dhamira ya Serikali ya kukuza uhuru wa vyombo vya habari ni pamoja na mchakato wa marekebisho ya sheria ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016, marekebisho yaliyowasilishwa na kusomwa bungeni kwa mara ya kwanza kupitia muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali mwezi Februari mwaka huu.

Send this to a friend