Nairobi: Google yatangaza nafasi za kazi zaidi ya 100

0
59

Google imetangaza nafasi za kazi zaidi ya 100 nchini Kenya baada ya kufungua kituo chake cha kwanza cha kuendeleza bidhaa (product development centre) Afrika kilichopo jijini Nairobi.

Hatua hiyo imetokana na uamuzi wa kampuni hiyo kuwekza $ 1 bilioni (TZS trilioni 2.3) Afrika ndani ya miaka mitano ijayo katika miradi ambayo itawezesha upatikanaji wa huduma za intaneti za kasi, uhakika na nafuu.

Katika kituo hicho Google inakusudia kuajiri ‘Engineering Manager, Product Manager, Software Engineer, Senior UX Designer au UX Researcher’.

Katika taarifa yake Google imeeleza kwamba inatafuta watu wenye vipaji, ubunifu ambao watawezesha kupatikana ufumbuzi wa changamoto za kiufundi kama vile kuboresha matumizi ya simu janja kwa watu barani Afrika au kuunda bidhaa zitakazowezesha ukuaji jumuishi wa wananchi.

Google inaungana na kampuni nyingine zinazolimulika soko la Afrika kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa intaneti ambao watakuwa vijana ifikapo mwaka 2030. Katika kipindi hicho, Afrika inakadiriwa kwamba itakuwa na watumiaji wa intaneti milioni 800 na moja ya tatu ya watu wote duniani walio chini ya umri wa miaka 35.

Taarifa zaidi kuhusu nafasi hizo tembelea Google: Africa Blog