Namna 5 ya kuepuka kupatwa na kiharusi

0
39

Wataalam wa afya wanasema asilimia 80 ya viharusi vinaweza kuzuiwa kupitia mabadiliko ya mtindo mzuri wa maisha na kucheki afya mara kwa mara ili kudhibiti hatari za kiharusi.

Watafiti wamegundua hatua nyingi ambazo watu wanaweza kuchukua ili kupunguza hatari ya kiharusi.

1.Ikiwa unavuta sigara, acha
Uchunguzi unaonesha kwamba kwa kila sigara tano mtu anazovuta kila siku, hatari ya kupata kiharusi huongezeka kwa asilimia 12. Kwa watu wazima uvutaji sigara huongeza hatari ya kiharusi maradufu ikilinganishwa na kutovuta sigara, utafiti wa 2020 uligundua.

 Sababu 6 za kwanini mtoto wako analia kwa muda mrefu usiku

2.Punguza unywaji wa pombe
Pombe inaweza kuongeza viwango vya shinikizo la damu. Kupunguza unywaji wako wa pombe kunaweza kupunguza hatari ya kiharusi. Wanaume hawapaswi kunywa zaidi  ya vinywaji viwili kwa siku, na wanawake hawapaswi kunywa zaidi ya moja kwa siku.

3.Kutana na daktari
Zungumza na daktari wako kuhusu hatua unazoweza kuchukua ili kupunguza hatari yako ya kiharusi.
Ikiwa una ugonjwa wa moyo, cholesterol ya juu, shinikizo la damu, au kisukari, unaweza kuchukua hatua za kupunguza hatari yako ya kiharusi.

4.Dhibiti kisukari
Ikiwa una ugonjwa wa kisukari, angalia viwango vya sukari yako ya damu mara kwa mara.

5.Mtindo wa maisha
Fanya mazoezi zaidi ya mwili au kuchagua vyakula bora zaidi. Hii itasaidia kuweka sukari yako ya damu chini ya udhibiti mzuri na kusaidia kupunguza hatari yako ya kiharusi.

Send this to a friend