Namna bora ya kuwadhibiti mende ndani kwako

0
97

Changamoto ya wadudu ndani ya nyumba yako husababishwa na mambo mengi lakini kubwa zaidi ni hali ya usafi na udhibiti taka katika maeneo yanayozunguka nyumba.

Unaweza kudhani ni wadudu tu lakini huenda haufahamu kuwa mende anaweza kusababisha changamoto za kiafya kwa wakazi na wageni wa nyumbani endapo hawatodhibitiwa.

Mende huacha vichochezi vya mzio hewani kupitia mate, kinyesi na kujivua sehemu za mwili wake (shedding). Haya yanaweza kuathiri mfumo wa upumuaji wa mtu hasa kama ana mzio na pumu.

1.Epuka kuacha vyombo vichafu vikizagaa
Kama wadudu wengine, mende nao hufika majumbani wakiwa wanatafuta chakula. Endapo wakija kwako na wakakuta umeacha vyombo vichafu, hisia yao ni kama mtu mwenye njaa kufika kwenye ardhi yenye chakula.

Ili kuepukana na hiyo, inashauriwa kuosha vyombo vyako baada ya kuvitumia hasa muda wa usiku. Usiviache vikizagaa.

2.Tumia bidhaa za kufukuza wadudu hasa makabatini
Wakati mwingine hawafuati chakula, wanafuata makazi na mara nyingi huwa ni chemba za vyooni au makabati.

Aina mbili za sababu za kutoa harufu mbaya kinywani

Ili kuepukana na hayo jaribu kutumia sukari ya unga, magamba ya mayai na majani yanayojulikana kama ‘baby leaves’. Vitu hivi vina harufu ambayo siyo rafiki kwa mende hivyo hawatokaa kabatini kwako.

3. Weka chombo cha taka mbali, ifunike kila mara
Mbali na kuvutia nzi nyumbani, ndoo za taka ambazo hazina mifuniko ni kivutio cha paka wa mitaani, nzi na hata wanyama wengine.

Ndoo ya taka ndani na hata nje ni kivutio pia cha mende hivyo hakikisha kama umeweka ndoo ya taka au mifuko ya taka hakikisha mara zote imefungwa vizuri.

4. Wataalamu wa usafi majumbani, wanashauri kupulizia dawa ya kuua wadudu wa nyumbani (fumigation) walau mara moja kila mwaka. Kupulizia dawa ni muhimu kwani uonapo mende mmoja nyumbani kwako ni ishara ya kuwa hayupo peke yake, wapo wenzie wengi waliojificha.

Kupulizia dawa ya wadudu itakusaidia kuwaua kabla hata hawajaanza kukusababishia adha kubwa.