Namna ngono ya mdomo inavyoeneza maambukizi ya UKIMWI

1
43

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya DARE, Dkt. Lilian Benjamin ameishauri jamii kuachana na ngono kwa njia ya mdomo kwa kuwa inachangia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Akizungumza katika semina kwa wahariri na waandishi wa habari, Dk. Lilian ameeleza kuwa ute unaopatikana chini ya fizi na maji yaliyopo kwenye sehemu za siri za mwanamke, vimethibitika kitaalam kuwa vinaweza kuwa na VVU, hivyo kufanya aina hii ya ngono kunaweza kuchangia maambukizi na madhara mengine.

Aidha, Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Nyangusi Laiser amesema majimaji yaliyoko mdomoni yanaweza kuwa na chembechembe za damu ikiwa mdomoni kuna michubuko, hivyo kama mtu ana VVU anaweza pia kumuambukiza mwenza wake.

Hata hivyo, Laiser amebainisha kuwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wanaongoza kwa maambukizi mapya VVU kwa asilimia 80.

Send this to a friend