Namna sahihi ya kujibu unapoulizwa udhaifu wako kwenye usaili wa kazi

0
34

Usaili wa kazi ni mchakato ambao waajiri wanatumia kuchagua waombaji bora kwa ajili ya nafasi za kazi. Hii ni hatua muhimu katika mchakato wa kuajiri na inaweza kujumuisha aina mbalimbali za maswali na majaribio ili kupima ujuzi, uzoefu, na sifa za waombaji.

Maswali yanayoulizwa kwenye usaili huandaliwa katika namna inayomwezesha msaili kupima uwezo na uelewa wa msailiwa katika masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya kazi aliyoimba.

Msailiwa anapaswa kuzingatia maswali yote anayoulizwa na kama kuna maswali ambayo hana uelewa nayo basi awe muwazi kwa wasaili.

Kipengele kinachohitaji umakini zaidi ni kwenye kuelezea udhaifu ulionao, pamoja na kwamba kila binadamu ana udhaifu wake, lakini ni wachache sana wenye ujasiri wa kukubali mapungufu hayo na kuwa tayari kujirekebisha.

Nchi 10 za Afrika zinazoongoza kwa ndoa za wake wengi

Msajili anaweza kuainisha udhaifu au upungufu alionao katika eneo la utendaji ambao hauna athari kubwa kwenye utekelezaji wa majukumu na kuonesha juhudi alizofanya kutatua upungufu huo.

Mfano unaweza kuelezea udhaifu katika kupokea kwa haraka mabadiliko ya kiteknolojia na uhitaji wa muda kidogo ili kuelewa mabadiliko hayo kabla ya kuanza kazi na kuyatekeleza katika eneo lako la kazi.

Mfano wa udhaifu huu hauna athari ya moja kwa moja kwenye utendaji, zaidi unaweza kutafsiriwa kama umakini wa msailiwa katika kuchunguza kwa kina mambo kabla ya kuyajumuisha katika utaratibu wake wa kazi.

Kuhusu ubora wa kikazi, msailiwa anaweza kujibu katika kufafanua kuhusu ujuzi, taaluma, uzoefu wa utendaji na mchango katika kuleta matokeo chanya kwa kampuni au taasisi anayotarajia kufanya kazi.

Send this to a friend