Namna ya kujilinda dhidi ya utekaji nyara na hali za hatari

0
23

Kila mtu ana jukumu la kuhakikisha usalama wake binafsi, hasa katika nyakati hizi ambapo vitendo vya uhalifu, kama vile utekaji nyara, vimeongezeka katika baadhi ya maeneo. Kujua namna ya kujilinda na kuchukua tahadhari mapema ni hatua muhimu katika kuzuia hali za hatari.

Hapa chini ni maelezo ya kina ya njia unazoweza kutumia kujilinda.

1. Epuka maeneo hatari

Usitembee peke yako usiku, hasa kwenye maeneo yasiyo na mwanga au watu na epuka njia za mkato kupitia vichochoro, misitu au maeneo ambayo si salama.

2. Wajulishe wapendwa wako unapokwenda

Kabla ya kutoka nyumbani, waambie marafiki au familia yako mahali unapokwenda na muda wa kurudi. Tumia teknolojia kama GPS au “location sharing” kushiriki eneo lako na mtu unayemwamini.

3. Zingatia dalili za hatari
Kama kuna gari lisilojulikana linakufuata, au mtu anakutazama kwa muda mrefu, songa haraka mahali penye watu. Usikubali mazungumzo na watu usiowajua hasa ikiwa wanaonekana kuwa na nia isiyo nzuri.

4. Usalama wa Simu
Hakikisha simu yako ina chaji na unaweza kuitumia wakati wowote wa dharura. Hifadhi namba za dharura kama polisi au msaada wa haraka.

5. Panga jinsi ya kujibu hali ya hatari
Fikiria hali za dharura na ujiandae jinsi utakavyopambana nayo. Jadiliana hili na watoto au wapendwa wako mara kwa mara. Chukua mafunzo ya kujilinda (self-defense) ili kujiandaa na hali ya kushambuliwa.

6. Beba vifaa vya kujilinda
Vifaa vidogo kama kipulizi cha machozi (pepper spray) vinaweza kusaidia kujikinga. Hakikisha unafuata sheria za eneo lako kuhusu matumizi ya vifaa vya kujilinda.

7. Kimbia na piga kelele
Ikiwa hali ya hatari inatokea, jaribu kukimbia haraka kwenda mahali salama. Wakati wa kukimbia, piga kelele kuelezea kinachoendelea. Mfano, sema “Naibiwa!” au “Nisaidie!” badala ya kupiga kelele bila maneno.

8. Epuka kupanda magari ya watu usiowajua
Usipande gari la mtu usiyemjua hata kama atadai anakufahamu au anaifahamu familia yako, kumbuka mtu mbaya hana alama usoni mwake.

9. Zingatia ujasiri
Onyesha ujasiri unapokuwa unatembea. Walengwa wa uhalifu mara nyingi ni wale wanaoonekana dhaifu au waliopotea. Angalia moja kwa moja mbele, tembea kwa kasi ya kawaida, na epuka kuonekana mnyonge.

10. Wasiliana na mamlaka haraka

Ikiwa unahisi uko hatarini, wasiliana mara moja na polisi au mamlaka husika. Ikiwezekana, tumia programu za simu za dharura ambazo zinaweza kusaidia kupiga simu kwa msaada haraka.

Send this to a friend