Namna ya kuzuia athari za mlipuko utokanao na gesi ya majumbani

0
47

Gesi ni nzuri kwa matumizi ya nyumbani, kwa sababu ni haraka zaidi kwa kupikia.

Pamoja na uzuri wake, pia ni hatari kama hautozingatia usalama wake.

Gesi hutoa kaboni yenye sumu na ambayo hushika moto haraka sana, hulipuka kama bomu, hivyo kuleta madhara ya haraka zaidi.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji limesema ukisafirisha mtungi wa gesi kwa ‘bodaboda’ ukiwa umeulaza, unatakiwa kuachwa kwa dakika 30 hadi dakika 45 kabla ya matumizi, kwa sababu unaweza kusababisha mlipuko.

Unaposafirisha mtungi wa gesi kwa  ‘bodaboda’ wengi huwa wanalaza mitungi, hivyo gesi inabadilisha mwelekeo,  na nyingi inakuwa imesogea katika eneo la mdomo hivyo ukiishusha na kuiwasha inaweza kuwa na moto mkali kuliko kawaida au kichwa kinaweza kufyatuka kutokana na kasi yake.

Maswali 7 ya kujiuliza kabla ya kuacha kazi yako

Watalaamu wanashauri,  kwa usalama zaidi mtungi wako wa gesi ya kupikia uweke nje ya nyumba na tumia mpira wa gesi kupeleka gesi kwenye jiko lenyewe la kupikia.

Pia, unashauriwa usitingishe mtungi wa gesi kutambua kama gesi imeisha ama bado, tumia kitambaa na  kiweke maji kisha paka kwenye huo mtungi kwa pembeni na utaona kiasi kilichobaki.

Usihifadhi vitu vya kupendeza kwa watoto karibu na lilipo jiko la kupikia, watoto wanaweza kupanda juu ya jiko au kuchezea na kusababisha madhara na  kujeruhiwa vibaya.

Utafanya nini ikiwa kuna uvujaji wa gesi nyumbani kwako?

1.Usiguse swichi yoyote ya umeme wala usijaribu kuwasha kifaa chochote cha umeme.

2.Fungua madirisha na milango ya nje mara moja ili kuruhusu gesi kutawanyika haraka iwezekanavyo.

3.Mwondoe kila mtu kutoka kwa jengo mara moja.

4.Piga simu kwa wasaidizi wa kitaalamu, piga simu kwa idara ya moto.

5.Usiruhusu mtu mwingine yeyote kuingia ndani isipokuwa mtaalam. Subiri kila kitu kiwe sawa kabla ya kurudi ndani.