Namna ya kukabiliana na maumivu ya jino ukiwa nyumbani

0
65

Sehemu ya ndani ya jino lako ni nyenzo laini iliyojaa neva, tishu na mishipa ya damu. Mishipa hii ni kati ya mishipa nyeti zaidi katika mwili wako hivyo inapoambukizwa na bakteria inaweza kusababisha maumivu makali.

Maumivu kwenye jino pia yanaweza kutokana na ugonjwa wa fizi, jino lililopasuka, kuvunjika au matatizo ya taya.

Unachoweza kufanya ukiwa na maumivu ya meno

Unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza maumivu ya jino wakati unasubiri kuonana na mtaalamu wa meno.

  • Sukutua mdomo wako kwa maji ya joto yenye chumvi. Maji ya chumvi yanaweza kulegeza uchafu katika meno yako na kupunguza uvimbe. Koroga kijiko cha chumvi kwenye glasi ya maji ya joto na suuza kinywa chako vizuri.
  • Weka mafuata ya karafuu ‘’clove oil’’ kwenye jino linalouma. Weka matone kadhaa kwenye pamba halafu iweke kwenye jino linaluma.
  • Meza dawa za kupunguza maumivu zilizoshauriwa na mtaalamu wa afya.
  • Kitunguu saumu. Katakata vipande vya kitunguu saumu uvitumie kwenye eneo lililoathiriwa. Kitunguu saumu kinaweza kuua bakteria (ina antimicrobial allicin) na kupunguza maumivu.

 

Jinsi ya kuepuka magonjwa ya meno

  1. Ondoa mabaki ya chakula kwa kusukutua mdomoni na maji baada ya kutoka kula, pamoja na kunywa maji mengi dakika 30 baada ya kutoka kula.
  2. Safisha meno yako hata mara mbili kwa siku.
  3. Epuka kula vyakula vyenye kemikali, vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi.

 

 

 

 

Send this to a friend