Nape aagiza watumiaji simu wasiungwe kwenye huduma ambazo hawajaziomba

0
40

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametoa maelekezo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni za mawasiliano ya simu nchini kutatua kero za watu kuunganishwa kwenye huduma ambazo hawakuziomba.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya tathmini ya hali ya mawasiliano pamoja na hatua mbalimbali zilizochukuliwa kufuatia malalamiko ya watumiaji wa huduma za mtandao za moja ya kampuni za simu nchini.

“Kumekuwa na kero kwa wananchi kuingizwa kwenye huduma ambazo hawakuziomba, TCRA na makampuni ya simu kaeni mtafute utatuzi walikomeshe hili mara moja,“ ameagiza Waziri Nape.

Rais Samia: Magari ya TASAF yasiende kubeba magunia ya mikaa

Aidha, ameilekeza TCRA na makampuni ya simu kukaa na kutatua malalamiko ya matumizi ya bando ambayo mtumiaji hajui limetumikaje, pia ameelekeza makampuni ya simu kuboresha programu tumizi (mobile application) ili isaidie kupunguza malalamiko ya watu kutojua wametumiaje data zao.

Send this to a friend