Nape awaonya matajiri wanaotumia fedha ili mitaa iitwe majina yao

0
42

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka matajiri wanaotumia fursa ya kuwajengea watu miundombinu au kutoa fedha kidogo ili mitaa iitwe majina yao kuacha tabia hiyo kwani siyo sahihi.

Ameyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Utangazaji TBC na kueleza kuwa anafahamu kuna baadhi ya maeneo yana migogoro na hakuna mtaa utakaochagulliwa jina na Serikali, hivyo vifanyike vikao vya Serikali za Mitaa na wakazi wote wa eneo husika wakubaliane jina la mtaa husika.

“Nimesikia kuna baadhi ya mitaa kuna watu wanaweka miundombinu au wanatoa fedha ili mitaa iitwe majina yao, tunayo majina mengi ya viongozi na mashujaa wetu, kabila na miji yetu, haya ndiyo yawe kipaumbele badala ya kuita mtaa mtu mwenye fedha, tunaweza kukuta mtaa mzima mtu ameweka majina ya Watoto wake,” amesema Nape.

Aidha, ameagiza iangaliwe namna ambayo itahakikisha majina ya mitaa yanaakisi asili ya eneo husika  au watu wake.

Pia, ameutaka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Miji na Vijijini (TARURA) kutumia nafasi ya uwekaji wa anwani za makazi na postkodi kuweka majina katika barabara zake zote ili kurahisisha mfumo huo.

Send this to a friend