Nauli mpya za mabasi zaanza kutumika leo

0
86

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza kuanza kutumika kwa nauli za mabasi ya masafa marefu na mijini (daladala) kuanzia Ijumaa Desemba 08, 2023.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na LATRA imesema hadi kumalizika siku 14 tangu amri ya Bodi ya LATRA itangazwe kwenye gazeti la Serikali Novemba 24, mwaka huu hakukuwa na pingamizi la kisheria dhidi ya amri hiyo.

“Watoa huduma wanakumbushwa kuzingatia amri ya Bodi ya LATRA pamoja na nauli halisi za ukomo kwa mabasi ya masafa marefu na mijini (daladala) ambazo pia zinapatikana katika tovuti ya LATRA,” imeeleza.

Imeongeza kuwa kifungu cha 19 cha sheria ya LATRA sura ya 413 kimeipa LATRA jukumu la kupanga na kufanya marejeo ya tozo za huduma ya Usafiri ikiwa ni pamoja na nauli za mabasi, hivyo wasafirishaji hawaruhusiwi kuzidisha bali wanaruhusiwa kutoza nauli ya chini ya ukomo uliowekwa kwa misingi ya ushindani.

Send this to a friend