Nauli za daladala zapanda. Hizi ni nauli mpya zilizotangazwa na LATRA

0
69

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli mpya ya mabasi ya mijini na masafa marefu ambapo safari ambazo hazizidi kilomita 10 gharama yake itakuwa TZS 600 badala ya TZS 500.

Safari zinazozidi kilomita 10, yaani kilomita 11 hadi kilimota 15 sasa itakuwa TZS 700 badala ya TZS 550, kilomita 16 hadi kilomita 20 nauli itakuwa 800 badala ya 600, kilomita 21 hadi kilomita 25 ambayo nauli yake ni TZS 700, nauli itakuwa TZS 900 na kilomita 26 hadi kilomita 30 nauli itakuwa TZS 1,100 kutoka TZS 850, kilomita 31 hadi kilomita 35 nauli itakuwa 1,300 badala ya 1,000 na kilomita 36 hadi kilomita 40 nauli itakuwa 1,400 badala ya 1,100.

Ametangaza mabadiliko hayo Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Suluo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha ikiwa ni mrejesho wa kikao kilichofanyika kati ya LATRA na wadau wa usafirishaji.

LATRA imesema kwa upande wa nauli za wanafunzi, gharama imebaki kuwa shilingi 200 kama hapo awali.

Aidha, LATRA imewaelekeza madereva kufuata taratibu na masharti yaliyotolewa ikiwemo kutotoza nauli iliyopendekezwa pamoja na kuzingatia usafi kwa kupulizia dawa ili kuua wadudu kwenye magari.