NBS yakanusha majina ya ajira za sensa yanayosambaa mtandaoni

0
47

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha orodha ya majina ya maombi ya kazi ya ajira za muda mfupi za sensa ya watu na makazi yanayosambaa mtandaoni kuwa si za kweli.

Ameyasema hayo Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka NBS, Dkt. Albina Chuwa wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma.

Dkt. Chuwa amesema taarifa hizo zinazosambaa mtandaoni si rasmi, hivyo Watanzania walioomba nafasi za ukarani na usimamizi wa sensa katika maeneno wanayoishi watapata taarifa kupitia maeneo yao.

“Watanzania wote wanatakiwa kujua kwamba taarifa yoyote kuhusu mwenendo wa maandalizi ya sensa ya watu na makazi, sensa ya majengo na sensa ya anuani za makazi ikiwemo ajira hizi za muda itatolewa na Serikali kupitia vyombo vya habari,” amesema Dkt. Chuwa

Send this to a friend