NCBA Bank Tanzania Limited yateua Mkurugenzi na Afisa Mkuu Mtendaji wapya
Bi. Margaret Karume mwenye uzoefu wa miaka 27 kwenye sekta ya benki
Dar es Salaam. NIC Bank Tanzania Ltd na CBA Bank Tanzania Ltd wapo mbioni kumalizia uunganaji wa taasisi zao na kuanza kutoa huduma zao kama NCBA Bank Tanzania Ltd. Wajumbe wa bodi teule wamemteua Bi. Margaret Karume atakaekua Mkurugenzi na Afisa Mkuu Mtendaji wa NCBA Bank (T) kuanzia tarehe 8 Julai benki itakapoanza kutoa huduma zake rasmi.
Kwa sasa Bi. Karume ni Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank Tanzania mwenye uzoefu wa miaka 27 katika sekta ya benki.
‘Huu ni ukurasa mpya kwa benki hizi mbili. Natazamia kufanya kazi na timu ya watu wenye nia moja ili kuimarisha taasisi yetu ya fedha nchini Tanzania. Taasisi hii mpya itaakisi dhamira na maadili kutoka benki zote mbili, baada ya kujifunza ubora wa pande zote na kujenga taasisi kubwa na bora ya kuwahudumia wateja na wadau wetu,’’ alinukuliwa Bi. Karume.
Katika vipindi tofauti, Bi. Karume amewahi kushikilia nyazfa mbalimbali katika sekta ya benki na kuwa kiongozi wa kuigwa katika ngazi zote za chini hadi juu za benki. Alipokuwa NIC Bank Group nchini Kenya amefanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Mikopo Hatarishi. Bi. Karume ana uzoefu imara na taaluma kwenye maendeleo ya fedha na biashara. Vilevile, ana utajiri na uzoefu katika kuhudumia wateja wakubwa wa kibenki uzoefu alioupata alipokuwa NIC Group plc na Barclays Bank Kenya (kwa sasa ABSA Bank).
Anashikilia shahada ya uzamili katika uratibu duniani (MBA ya Global Executive) na Shahada ya Sayansi (BSc). Alihitimu elimu ya utawala wa ngazi ya kibiashara kimataifa kutoka United States International University (USIU) – Africa na stashahada ya usimamizi wa mahusiano ya wateja kutoka Taasisi ya Kifedha (Uingereza). Vilevile, yeye ni mwanachama wa Taasisi ya Masuala ya Kifedha, Kenya.
Akithibitisha uteuzi wake, mwenyekiti mteule wa bodi ya NCBA Bw. Sharmapal Aggarwal alimpongeza Bi. Karume kwa kuteuliwa kwake.
‘Tunatambua uzoefu wake mkubwa kwenye sekta ya benki na tunasifu kwa kujitoa kwake upya kwenye benki. Tunaamini kuwa yeye ni mtu sahihi kuiongoza Benki ya NCBA kwenye zama mpya ya maendeleo endelevu na kuleta mafanikio kwa wadau wote Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla,’’ alinukuliwa. Vilevile alibainisha kuwa Bw. Gift Shoko ambaye ni Afisa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CBA Tanzania ni mteule katika bodi ya benki ya NCBA kama Mtendaji Mkuu, na ameteuliwa kuiongoza taasisi mpya kama Mkurugenzi Mtendaji wa biashara za kidijitali na wateja wadogo na wakubwa
Nafasi yake itaiongoza benki ya NCBA kwenye biashara za kidijitali ambapo ni kiini cha ukuaji endelevu wa biashara ya kundi hili wakati inalenga kuwa benki inayoongoza kwenye kanda katika miaka mitano ijayo.
“Kuleta benki zote mbili pamoja imetuwezesha kukua na kuwa benki kubwa katika sekta ya digitali. Kadri ambavyo teknolojia inaendelea kukua tunashuhudia teknolojia ikiwa inachukua nafasi muhimu zaidi katika kuleta ushirikishwaji wa kifedha nchini Tanzania, Afrika Mashariki na kwa bara zima kwa ujumla. Tuna vifaa, rasilimali na wataalamu wa kutuwezesha kuongoza katika soko, “Alisema Bwana Shoko.
–MWISHO–
KUHUSU NCBA BANK (T) LTD
Benki ya NCBA Bank (T) Limited ni muunganiko wa NIC Bank (T) Ltd na CBA Bank (T) Ltd. Uunganaji huu umewezeana kupitia ununuzi wa mali na dhima zote za CBA kwenda NIC.
Taarifa ya uhamishaji wa mali na dhima ulichapishwa na gazeti la Serikali tarehe 17 Januari 2020 (kama GN No. 48) na Magazeti mbalimbali nchini. Taarifa ya kuhamishwa kwa mali na dhima ilitolewa sambamba na na kifungu cha 4 cha Transfer of Businesses (Protection of Creditors) Act, Cap 327 R.E 2002.
Benki Kuu ya Tanzania iliidhinisha leseni ya benki iliyotoa ruhusa kwa taasisi hizi mbili kuanzisha huduma zao rasmi kama NCBA Bank (T) Ltd.
Muunganiko huu utaifanya benki hii kuwa kubwa zaidi kwenye huduma za kifedha kwenye kanda, benki yenye nguvu kifedha, utaalamu, na kupanuka kwa msaada kikanda nchini Tanzania na mikoani, kukuza uchumi na kukidhi matarajio.
Kundi hili litaimarisha sekta ya benki na kuwa mdau mkubwa wa ukuaji wa uchumi nchini Tanzania, kwenye kanda na zaidi.
Ubora wa pamoja utachochea biashara za wateja wadogo na wakubwa katika benki na ukuaji imara katika kila njanja ya benki na usimamizi mali.
Taasisi hii mpya itakuwa benki ya kila mtu itakayotosheleza mahitaji ya idadi kubwa ya wateja tofauti kwa kuwahudumia bidhaa na huduma mbalimbali kwenye mashirika, taasisi, biashara ndogo na kati na wateja wote wa huduma za kibenki ambao watafaidika na uhusiano imara kwenye usimamizi na huduma bora kwa wateja.
Benki ya kimataifa kutoka Afrika inayojivunia kufanya kazi katika viwango vya kimataifa, benki ya NCBA hadi sasa ni;
• Benki inayoongoza kwa idadi kubwa ya wateja wengi ikiwa na wateja zaidi ya milioni 40 barani Afrika na kwenye kanda ikiwa na uwezo thabiti kwenye utoaji huduma za kidijitali, wateja wakubwa na utoaji fedha za mali.
• Miongoni mwa taasisi kubwa zaidi ya kifedha ukanda wa Afrika Mashariki na benki ya tatu kwa ukubwa nchini Kenya ikiwa na mtaji wa mali zaidi ya KES 444 bilioni (Tsh 9,324bn) na mtaji sawa kwa wanahisa KES 65 Bilioni (Tsh 1,365).
KWA TAARIFA ZAIDI
NCBA Bank Tanzania
Caroline Maajabu Mbaga
Head; Marketing, Communications & Citizenship
Email: caroline.mbaga@nicgroup.com
Tel: +255 (22) 2295000 / DL: +255 768 987008