NCCR-Mageuzi: Dkt. Slaa na wenzake wasikichafue chama chetu

0
44

Kufuatia sintofahamu iliyojitokeza ikihusisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha NCCR- Mageuzi ambapo CHADEMA imedai NCCR- Mageuzi iliandaa mkutano katika jimbo la Busokelo mkoani Mbeya ikitumia nyimbo zake kuita wanachama, Chama cha NCCR- Mageuzi kimesema chama hicho hakiutambui mkutano huo na walioandaa mkutano huo si viongozi wa chama.

Akizungumza na vyombo vya Habari, Makamu Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, Joseph Selasini amesema kikundi cha Sauti ya Watanzania kikiongozwa na Dkt. Wilbroad Slaa na wenzake kimeamua kumtumia kinyemela Wakili Boniphace Mwabukusi ili kufanikisha mkutano huo, na kuomba Jehi la Polisi kutoruhusu mkutano wowote wa chama hicho pasipo idhini ya katibu mkuu wa chama.

“Nimesikia kwamba huo mkutano ulihutubiwa na Mwabukusi, Mwabukusi ni mwanachama wetu, lakini nafasi zake zote za uongozi ziliondolewa na mkutano wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu mwaka jana, kwahivyo kama alikwenda na kufanya huo mkutano, kama kiongozi wa NCCR- Mageuzi nataka Watanzania waelewe hivyo kwamba yeye siyo kiongozi na haya anayoyafanya tumeanza kuyajadili,” amesema.

Tanzania kuuza sukari nje ya nchi miaka miwili ijayo

Ameongeza, “na sisi tunataka kuwaambia wasichafue chama chetu, waendelee na mipango yao. Sisi tunawaagiza wanachama wetu, kuanzia leo ni marufuku kuhitisha mikutano ya hadhara yeyote mahali popote bila kwanza kuwasiliana na ofisi ya katibu mkuu. NCCR- Mageuzi tusigombanishwe na wanachama wetu.”

Hata hivyo mkutano huo ulizuiwa na jeshi la polisi kufanyika baada ya kupokea malalaniko yaliyotolewa na CHADEMA.

Send this to a friend