NCCR Mageuzi yamsimamisha Mbatia

2
15

Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia na Makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shughuli zozote za chama hadi pale mkutano mkuu utakapoitishwa ili kujieleza kuhusu tuhuma zinazowakabali.

NCCR- Mageuzi imefanya uamuzi huo leo Mei 21, 2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu.

Aidha, Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini amesema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa.

Hata hivyo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Sisty Nyahoza amesema walipokea barua kutoka NCCR-Mageuzi kuwa kuna mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhamini pamoja na ajenda ya kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara, hivyo wanasubiri barua rasmi ili kutoa taarifa.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend