Nchi 10 Afrika zenye gharama kubwa zaidi za intaneti

0
38

Nchi 10 Afrika zenye gharama kubwa zaidi za intaneti

 Kwa mujibu wa Business Insider Africa, hizi ni nchi 10 za Afrika zenye gharama kubwa zaidi ya intaneti

 Equatorial Guinea inaongoza katika orodha hiyo.

Kulingana na takwimu za Statista zilizotolewa Disemba 2021, zimeonesha takribani Waafrika milioni 480 wanatumia mitandao ya simu, huku ikitoa orodha ya nchi za Afrika zenye bei ghali zaidi za data ya simu.

Chanzo cha gharama hizo kimeelezwa kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa miundombinu na ushuru mkubwa katika sekta ya mawasiliano ya simu barani Afrika.

Hizi ni nchi 10 za Afrika zenye bei ghali zaidi za data ya simu. Kipimo kipo kwa gigabyte moja;

1. Equatorial Guinea: Nchi hii kwa sasa ina bei ghali zaidi ya data ya simu, huku Gigabyte moja ikigharimu $49.67 (Sawa na TZS 115,830.44).

2. São Tomé and Principe: Gigabyte moja inagharimu $30.97 (Sawa na TZS 72,222.04).

3. Malawi: Malawi ni nchi ya tatu yenye bei ghali zaidi ya data ya simu barani Afrika, ikilipia $25.46 (Sawa na TZS 59,372.72) kwa Gigabyte.

4. Chad: Chad inalipia $23.33 (Sawa na TZS 54,405.56).

5. Namibia: Gigabyte moja inagharimu $22.37 (Sawa na TZS 52,166.84).

6. Jamhuri ya Afrika ya Kati: Gigabayte moja ni $9.03 (Sawa na TZS 21,057.96).

7. Ushelisheli: Gigabyte moja inagharimu $8.64 (Swa na TZS 20,148.48).

8. Gambia: Bei ya wastani ya data ya Gigabyte nchini Gambia ni $5.86 (Sawa na TZS 13,665.52).

9. Mauritania: Gigabyte moja inagharimu $5.56 (Sawa na TZS 12,965.92).

10. Madagaska: Gigabayte moja ni $5.14 (Sawa na TZS 11,986.48).

Nchini Tanzania, kupitia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Tanzania ni nchi ya 6 kwa bara la Afrika, na ni nchi ya 50 duniani kwa kuwa na gharama ndogo za usafirishaji data.

Send this to a friend