Nchi 10 Afrika zinazodaiwa zaidi na China

0
40

Athari za kiuchumi za janga la UVIKO-19 na vita vya Urusi na Ukraine vimefanya iwe vigumu zaidi kwa nchi nyingi za Afrika kulipa madeni yao. Sasa, mataifa 22 ya Afrika yanakabiliwa na mzozo wa madeni au yako katika hatari kubwa ya kukumbwa nayo.

China ni mkopeshaji mkuu wa mataifa mengi ya Afrika, lakini mikopo yake imeshuka katika miaka ya hivi karibuni, hali inayotabiriwa kuwa mbaya kwa mwaka 2023 na kupunguza uwezo wa mataifa ya Afrika kupata fedha zinazohitajika ili kufanya uboreshaji wa kijamii kwa watu wao na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Aina 6 za ‘Smartphones’ bora zaidi unazoweza kununua

Mwaka 2020 mataifa saba ya Kiafrika yaliripotiwa na Benki ya Dunia kuwa katika matatizo ya kifedha au hatari ya kuelemewa na madeni kutokana na wingi wa ufadhili wa China.

Zifuatazo ni nchi 10 za Afrika zinazodaiwa zaidi na China kwa mujibu wa Business Insider Africa;

No Nchi Kiwango cha madeni (TZS)
01 Angola Trilioni 99.7
02 Ethiopia Trilioni 32.12
03 Zambia Trilioni 23.03
04 Kenya Trilioni 21.5
05 Nigeria Trilioni 15.7
06 Cameroon Trilioni 14.5
07 Sudan Trilioni 14.4
08 DR Congo Trilioni 12.6
09 Ghana Trilioni 12.4
10 Cote d’Ivoire Trilioni 8.7

 

 

 

 

Send this to a friend