Nchi 10 za Afrika zenye bei kubwa zaidi ya mafuta

0
40

Dunia imepata wakati mgumu kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta. Athari za mabadiliko haya katika sekta za uchumi, na watumiaji wa kawaida ni kubwa.

Kama vile uchumi wa nchi nyingine duniani, uchumi wa Afrika unakabiliwa na matokeo mabaya ya ongezeko la bei ya mafuta. Bei ya mafuta ina athari kubwa katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na usafirishaji, ustawi wa kijamii, ukuaji wa kiuchumi na mfumuko wa bei.

Kulingana na ripoti za hivi karibuni, gharama kubwa ya mafuta imesababisha mivutano katika nchi kadhaa barani Afrika. Kutokana na bei za gesi kupanda, nchi kama Kenya imekumbana na maandamano mengi, pia kuleta athari kubwa kwa Nigeria ambayo hivi karibuni imefuta ruzuku ya mafuta.

Hii ni orodha ya nchi 10 za Afrika zenye bei (TZS) kubwa zaidi za petroli, iliyotolewa na GlobalPetrolPrices.com (kwa lita).

1.Afrika ya Kati: 4,577
2.Malawi: 4,125
3.Senegal: 4,120
4.Zimbabwe: 3,903
5.Seychelles: 3,846
6.Mauritius: 3,796
7.Morocco: 3,781
8.Cape Verde: 3,632
9.Mali: 3,602
10.Burkina Faso: 3,538

Send this to a friend