
Idadi kubwa ya mataifa ya Afrika yanajikuta yakikabiliwa na hali ngumu ya kifedha kutokana na mzigo mkubwa wa madeni wanayodaiwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Nchi kama Ghana na Malawi zimekuwa zikitekeleza mipango inayoungwa mkono na IMF, lakini mara nyingi mipango hiyo imeambatana na hatua kali za kubana matumizi ambazo huibua hasira za wananchi, hata kama lengo lake ni kuleta uthabiti wa muda mrefu wa kiuchumi.
Madeni haya ya IMF, ambayo kwa kawaida hukopwa ili kuziba nakisi ya bajeti, kuongeza akiba ya fedha za kigeni, au kuokoa uchumi wakati wa misukosuko mikali, sasa yamegeuka kuwa tishio kubwa.
Nchi yenye deni kubwa kwa IMF huwa inajikuta ikilazimika kutekeleza masharti magumu na mara nyingine yanayogusa masuala nyeti ya kisiasa, hali inayoweza kuvuruga uthabiti wa ndani na kuathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Hii ni orodha ya nchi 10 za Afrika zenye deni kubwa IMF hadi kufikia Juni 2025;
- Misri: Trilioni 20.6
- Kenya: Trilioni 7.7
- Angola: Trilioni 7.05
- Ghana: Trilioni 6.3
- Cote d’Ivoire: Trilioni 6.5
- DRC: Trilioni 4.6
- Ethiopia: Trilioni 3.6
- Cameroon: Trilioni 3.0
- Tanzania: Trilioni 2.6
- Senegal: Trilioni 2.5
Chanzo: IMF








