Nchi 10 za Afrika zenye deni kubwa zaidi IMF

0
71

Shirika la Fedha Duniani (IMF) limechapisha orodha ya nchi 10 za Afrika zenye deni kubwa zaidi, huku Tanzania ikiwa haijatajwa kwenye orodha hiyo hali iliyotafsiri kama uwepo wa ufanisi katika usimamizi wa bajeti na sera zake za kiuchumi.

Orodha ya IMF imekuwa kipimo muhimu cha kutathmini ya ukuaji wa uchumi na uimara wa kifedha kwa mataifa kote barani Afrika.

Mataifa haya yamekuwa yakipitia changamoto kubwa za kiuchumi zilizochangiwa na janga la UVIKO-19, ambalo lilisababisha kuongezeka kwa ukopaji ili kupunguza athari za mzozo huo kwa uchumi.

Nchi 10 za Afrika zenye idadi kubwa ya lugha

Tanzania kutokuwepo kwenye orodha ya nchi zenye madeni makubwa inaweza kutafsiriwa kama ishara chanya kwa wawekezaji na taasisi za fedha za kimataifa, ikionyesha kwamba viwango vya madeni ya Tanzania ni endelevu na vinaweza kudhibitiwa ikilinganishwa na nchi nyingine.

Hizi ni nchi 10 za Afrika zenye deni kubwa IMF, kulingana na tovuti rasmi ya IMF 2023;

Misri: TZS trilioni 30.1
Angola: TZS trilioni 7.9
Afrika Kusini: TZS trilioni 6.7
Côte d’Ivoire: TZS trilioni 5.3
Kenya: TZS trilioni 5.2
Nigeria: TZS trilioni 4.6
Ghana: TZS trilioni 4.1
Morocco: TZS trilioni 3.7
DR Congo: TZS trilioni 3.25
Tunisia: TZS trilioni 3.2