Nchi 10 za Afrika zenye furaha zaidi mwaka 2025

0
5

Furaha ni hisia ya utulivu na kuridhika inayotokana na hali nzuri ya maisha, mafanikio, au upendo kutoka kwa wengine. Lakini ukweli ni kwamba si kila nchi inatoa mazingira ambayo watu wanahisi kuridhika na kutosheka.

Wakati baadhi ya mataifa yanashika nafasi za juu kila mara katika Ripoti ya Furaha ya Dunia, mengine yanakabiliwa na changamoto kubwa zinazofanya maisha kuwa magumu kwa raia wao.

Kila mwaka, ripoti hii hutoa taswira ya ustawi wa dunia, ikionesha ni nchi zipi zinafanikiwa na zipi zinakumbwa na matatizo makubwa.

Ripoti ya hivi karibuni ya Furaha ya Dunia mwaka 2025, imeonesha kati ya mataifa ya Afrika, Mauritius inaongoza kama nchi yenye furaha zaidi, ikiwa nafasi ya 78 duniani, Libya inafuatia kwa nafasi ya 79, huku Algeria ikiwa nafasi ya 84.

Zifuatazo ni nchi 10 bora zaidi zenye furaha barani Afrika mwaka 2025 kwa mujibu wa Ripoti ya Furaha ya Dunia;

  1. Mauritius
  2. Libya
  3. Algeria
  4. Afrika Kusini
  5. Mozambique
  6. Gabon
  7. Côte d’Ivoire
  8. Congo
  9. Guinea
  10. Namibia