Nchi 10 za Afrika zenye gharama kubwa ya umeme kwa mwaka 2023

0
44

Kulingana na Yahoo Finance, soko la umeme duniani kwa sasa lina thamani ya zaidi ya $1.94 trilioni [quadrilioni 4.8] na inakadiriwa kufikia $3.9 trilioni [quadrilioni 9.8] mwaka 2032.

Makadirio hayo ni matokeo ya kuongezeka kwa mahitaji ya umeme, yanayotarajiwa kuongezeka kwa ongezeko la asilimia 3.3 kila mwaka.

Ukuaji huu unategemea ongezeko la idadi ya watu na maendeleo ya kiuchumi, huku sekta za viwanda, makazi, na biashara zikitarajiwa kuwa watumiaji wakubwa wa umeme.

Kwa hivyo, ni muhimu kwa Afrika kushughulikia changamoto katika sekta ya nishati ili kupunguza gharama na kuongeza mapato.

Ingawa Afrika inajivunia gharama nafuu ya umeme kimataifa, bado kuna maeneo yanayolipa bei kubwa ikilinganishwa na kipato cha kaya.

Hii ni orodha ya nchi za Afrika mwaka 2023 zenye bei ya juu zaidi ya umeme kwa kilowati kwa saa;

  1. Cabo Verde: TZS 794.7
  2. Mali: TZS 550.7
  3. Rwanda: TZS 520.6
  4. Burkina Faso: TZS 518
  5. Gabon: TZS 515.6
  6. Togo: TZS 487.9
  7. Senegal: TZS 460.2
  8. Kenya: TZS 432.6
  9. Uganda: TZS 427.5
  10. Sierra Leone – TZS 389.8
Send this to a friend