Nchi 10 za Afrika zenye huduma bora za Polisi
Ripoti ya Afrobarometer iliyochapishwa hivi karibuni, imebaini kuwa huduma za polisi barani Afrika zinakabiliwa na changamoto kubwa za uadilifu na weledi, huku asilimia ndogo ya raia wakiridhika na utendaji wa vyombo hivyo vya usalama.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyokusanya maoni ya raia kati ya mwaka 2021 na 2023, ni mmoja tu kati ya Waafrika watatu anayesema anaridhishwa na utendaji wa polisi.
Zaidi ya hayo, kati ya wale waliotafuta msaada wa polisi katika kipindi cha mwaka mmoja wa uchunguzi, asilimia 54 wamesema ilikuwa rahisi kupata msaada waliouhitaji. Hata hivyo, ripoti hiyo imeonesha upande mwingine wa utendaji wa polisi, ambapo asilimia 36 ya wahojiwa waliripoti kulazimika kutoa rushwa ili kupata huduma.
Takwimu hizo zinaonyesha changamoto kubwa zinazovikabili vyombo vya polisi barani Afrika, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uaminifu miongoni mwa raia na suala sugu la rushwa, ambalo linaendelea kudhoofisha juhudi za kulinda usalama na haki za watu wa kawaida.
Zifuatazo ni nchi 10 za Kiafrika zenye huduma bora za Polisi;
- Botswana
- Afrika Kusini
- Benin
- Tunisia
- Senegal
- Sao Tome na Principe
- Seychelles
- Ghana
- Cape Verde
- Lesotho
Chanzo: Business Insider Africa