Nchi 10 za Afrika zenye idadi kubwa ya lugha

0
47

Lugha ni mfumo wa mawasiliano unaotumia ishara, sauti, au maandishi kwa kusudi la kuwasiliana. Barani Afrika, kuna utajiri wa lugha ikiwa na zaidi ya lugha 2,000 zinazozungumzwa.

Miongoni mwa lugha kuu za Kiafrika ni Kiswahili ambacho kinazungumzwa zaidi Kusini na Mashariki mwa bara na Kihausa ni lugha kuu kwa watu wa Chadic nchini Nigeria, Niger, na Chad wakati Kiyoruba kikizungumzwa Kusini Magharibi mwa Nigeria, Benin, na Togo.

Pia, lugha za kigeni kama Kiingereza na Kifaransa zinazungumzwa sana na kutumika sehemu mbalimbali za bara, hasa kutokana na athari za kihistoria za ukoloni. Kwa mfano, lugha ya Kiingereza inazungumzwa na takribani Waafrika milioni 130, na ni lugha rasmi au ya pili katika nchi 27 kati ya 54 kwenye bara hilo.

Zifuatazo ni nchi 10 za Kiafrika zenye idadi kubwa zaidi ya lugha;

1 Nigeria: 520
2 Cameroon: 227
3 DR Congo: 214
4 Chad: 129
5 Tanzania: 128
6 Ethiopia: 92
7 Côte d’Ivoire: 88
8 Ghana: 83
9 Sudan: 75
10 Sudan Kusini: 73

Send this to a friend