
Afrika imeelezwa kuwa moja ya kanda zinazokua kwa kasi zaidi katika ustawi binafsi duniani, licha ya baadhi ya nchi kubwa kukabiliwa na changamoto za mgawanyo wa kipato na mali.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Utajiri Afrika 2025 iliyotolewa na Henley & Partners kwa kushirikiana na New World Wealth, idadi ya mamilionea barani humo inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 65 ndani ya muongo mmoja ujao.
Afrika yenye watu zaidi ya bilioni 1.5 na uchumi unaotarajiwa kufikia dola trilioni 29 ifikapo mwaka 2050, inatajwa kuzalisha mamilionea wapya kwa kasi inayokaribiana na masoko makubwa ya Asia na Mashariki ya Kati.
Hizi ni nchi 10 za Afrika zenye mamilionea wengi kwa mwaka 2025 (dola milioni 1+);
- Afrika Kusini: 41,100
- Misri: 14,800
- Morocco: 7,500
- Nigeria: 7,200
- Kenya: 6,800
- Mauritius: 4,800
- Algeria: 2,700
- Ghana: 2,600
- Namibia: 2,500
- Ethiopia: 2,400
Chanzo: Business Insider Africa







