Nchi 10 za Afrika zenye idadi kubwa ya ndege mwaka 2024

0
98

Sekta ya anga barani Afrika inaendelea kukua kwa kasi kubwa na kutengeneza fursa nyingi za maendeleo kupitia biashara na utalii.

Mahitaji ya usafiri wa anga yameongezeka, hivyo mashirika ya ndege yanajibu kwa kuongeza idadi ya safari na kupanua mitandao yao ili kukidhi mahitaji ya wateja. Hii inaweza kuonekana kupitia ununuzi wa ndege mpya, kuboresha huduma kwa abiria, na kuongeza njia mpya za ndege.

Boeing inatabiri kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya abiria wa ndani barani Afrika katika miongo miwili ijayo, huku idadi ikitarajiwa kupanda zaidi ya mara nne.

Nchi 10 za Afrika zenye kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira mwaka 2024

Ukuaji wa trafiki ya anga barani Afrika unatarajiwa kuongezeka kwa kiwango cha asilimia 7.4, ikiorodheshwa kama ya tatu kati ya maeneo ya kimataifa yenye ukuaji mkubwa zaidi na hivyo kuzidi kiwango cha wastani wa ukuaji wa kimataifa wa asilimia 6.1.

Zifuatazo ni nchi za Afrika zilizo na idadi kubwa ya ndege mwaka 2024 kulingana na Planespotters;

1 Afrika Kusini: 195
2 Kenya: 177
3 Misri:166
4 Ethiopia:142
5 Nigeria:140
6 Algeria: 80
7 Morocco: 64
8 Libya: 56
9 Angola: 41
10 Tunisia: 40

Tanzania kwa upande wake leo imepokea ndege nyingine Boeing 737-9 ambayo imeifanya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kufikisha ndege mpya 14 ambazo zimenunuliwa tangu mwaka 2016.