Nchi 10 za Afrika zenye idadi kubwa ya wanawake Serikalini

0
45

Ni ukweli usiopingika kwamba wanawake na wanaume bado hawana haki sawa duniani, ikiwa ni pamoja na nchi nyingi za Afrika.

Ripoti ya hivi karibuni imeeleza kuwa hakuna nchi duniani inayowapa wanawake fursa sawa na wanaume katika nafasi za kazi.

Hata hivyo, dunia imegundua umuhimu wa wanawake katika kujenga jamii za haki na endelevu na nchi za Afrika pia zinazidi kusimamia usawa wa kijinsia katika siasa japokuwa bado juhudi inahitajika lakini kumekuwa na matokeo mazuri.

Nchi 10 za Afrika zenye kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira mwaka 2024

Kulingana na Muungano wa Mabunge ya Kimataifa (IPU), Rwanda imeibuka kinara wa kimataifa katika masuala ya uwiano wa kijinsia, ikiwa na asilimia 61.3 ya wanawake katika bunge lake.

Zifuatazo ni nchi 10 za Afrika zenye idadi kubwa ya wanawake serikalini;

  1. Rwanda: 61.3%
  2. Senegal: 46.1%
  3. Afrika Kusini: 45.8%
  4. Namibia: 44.2%
  5. Msumbiji: 43.2%
  6. Ethiopia: 41.3%
  7. Cabo Verde: 38.9%
  8. Angola: 38.6%
  9. Burundi: 38.2%
  10. Tanzania : 37.4%
Send this to a friend