Ukosefu wa ajira ni moja ya changamoto kubwa barani Afrika, inayozuia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii.
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeonya kwamba ikiwa mambo hayatabadilika hivi karibuni, takriban vijana milioni 100 wanaweza kukosa ajira ifikapo mwaka 2030.
Kati ya vijana milioni 8 na 11 wanatazamiwa kujiunga na soko la ajira kila mwaka katika miongo ijayo, lakini ajira rasmi zinazoundwa kila mwaka ni takriban milioni 3 pekee, hivyo pengo ni kubwa.
Ripoti ya Statista imesema kuwa Afrika Kusini inashikilia kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira barani Afrika kwa asilimia 29.83, ikifuatiwa na Djibouti kwa asilimia 27.85.
Zifuatazo ni nchi 10 za Kiafrika zenye kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira;
1. Afrika Kusini: 29.83%
2. Djibouti: 27.85%
3. Eswatini: 24.65%
4. Gabon: 21.35%
5. Congo: 21.26%
6. Botswana: 20.72%
7. Somalia: 20.53%
8. Namibia: 20.37%
9. Libya: 20.07%
10. Sudan: 18.05%
Chanzo: Business Insider Africa