Nchi 10 za Afrika zenye kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira mwaka 2024

0
84

Ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa inayokabili uchumi wa bara la Afrika. Ingawa bara hili lina rasilimali nyingi za asili pamoja na ujuzi, fursa za ajira hazitoshi kwa idadi kubwa ya watu kutokana na uchumi dhaifu na ongezeko la idadi ya watu.

Vijana wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya ukosefu wa ajira, na takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana kinakaribia asilimia 11 japokuwa Serikali zimechukua hatua kadhaa kupambana na tatizo hili.

Pia kuna tofauti za kijinsia katika soko la ajira, ambapo takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kwa wanawake ni kikubwa zaidi kuliko kwa wanaume licha ya kuwa na ujuzi na uzoefu sawa.

Zifuatazo ni nchi 10 za Kiafrika zilizo na kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira katika 2024;

  1. Afrika Kusini: 32.1%
  2. Djibouti: 27.9%
  3. Eswatini: 24.65%
  4. Gabon: 21.35%
  5. Congo: 21.3%
  6. Botswana: 20.72%
  7. Somalia: 20.53%
  8. Namibia: 20.37%
  9. Libya: 20.07%
  10. Sudan: 18.05%

Chanzo: Business Insider

Send this to a friend