Nchi nyingi zinakabiliwa na changamoto za kiuchumi ambazo mara nyingine husababisha kutafuta msaada kutoka kwa taasisi kama Shirika la Fedha Duniani (IMF), ambapo huchukuliwa kama suluhisho la mwisho kuinua uchumi wa nchi pindi unapotetereka.
Mkopo kutoka IMF unaweza kuimarisha imani ya nchi hiyo katika macho ya wawekezaji wa kigeni. Kuongezeka kwa imani hii kunaweza kusababisha ongezeko la uwekezaji wa moja kwa moja wa nchi za kigeni na upatikanaji bora wa masoko ya mtaji duniani.
Hata hivyo, mikopo hii ikiwa haiongozwi au kutumiwa ipasavyo, inaweza kuathiri uchumi, kwani madeni yanaweza kusababisha mdororo wa kifedha katika uchumi wa nchi.
Hapa kuna orodha ya nchi 10 za Afrika zenye madeni makubwa kwa IMF, kwa mujibu wa tovuti rasmi ya IMF;
- Misri: TZS trilioni 29.9
- Angola: TZS trilioni 7.9
- Afrika Kusini: TZS trilioni 6.7
- Côte d’Ivoire: TZS trilioni 5.3
- Kenya: TZS trilioni 5.2
- Nigeria: TZS trilioni 4.6
- Ghana: TZS trilioni 4.1
- Morocco: TZS trilioni 3.7
- DR Congo: TZS trilioni 3.2
- Tunisia: TZS trilioni 3.1