Nchi 10 za Afrika zenye matumizi makubwa ya bangi

0
69

Uchunguzi wa hivi karibuni kuhusu matumizi ya bangi katika nchi za Kiafrika, unaonesha uwepo wa viwango vingi vya matumizi. Kwa kiwango cha kimataifa, asilimia 15 ya wakazi wa Marekani, Canada, Nigeria na Australia wenye umri wa miaka 15 na zaidi wamekiri kutumia bangi.

Ripoti ya hivi karibuni inaonesha ongezeko la viwango vya uvutaji sigara miongoni mwa watu wazima pamoja na kuongezeka kwa matumizi miongoni mwa vijana huku Nigeria ikiongoza ikiwa na idadi kubwa zaidi ya watumiaji wa bangi.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2021 kuhusu matumizi ya bangi, inatabiri kuongezeka kwa kiasi kikubwa karibu asilimia 40 ya idadi ya watumiaji wa dawa barani Afrika ifikapo mwaka 2030.

Kwa kutumia takwimu kutoka Ripoti ya Kimataifa ya Bangi, inaonesha nchi za Kiafrika zenye watumiaji wengi wa bangi;

1. Nigeria – milioni 20.8
2. Ethiopia – milioni 7.1
3. Misri – milioni 5.9
4. DR Congo – milioni 5
5. Tanzania – milioni 3.6
6. Kenya – milioni 3.3
7. Sudan – milioni 2.7
8. Uganda – milioni 2.6
9. Madagascar – milioni 2.1
10. Ghana – milioni 2

Chanzo: Business Insider

Send this to a friend