Nchi 10 za Afrika zenye ubora wa chini wa elimu

0
33

Elimu ni moja ya nguzo muhimu za maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii. Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo, ubora wa elimu umekuwa ukishuka kwa kiasi kikubwa, na kuathiri uwezo wa watu kufikia malengo yao ya kimaisha.

Ubora wa chini wa elimu una athari kubwa katika kila nyanja ya maisha ya binadamu, kuanzia katika maendeleo ya kiuchumi hadi katika ustawi wa kijamii na kisiasa. Makala hii inachambua sababu za ubora wa chini wa elimu na athari zake katika jamii.

Ingawa tatizo hili linaonekana kuwa la kudumu barani Afrika, kuna hatua zinazochukuliwa na serikali na washirika binafsi kupambana na matatizo hayo ili kukuza elimu barani Afrika.

Hizi ni nchi 10 bora za Kiafrika zenye ubora wa chini wa elimu kwa mujibu wa ripori ya Mo Ibrahim Foundation’s Financing Africa;

1. Afrika Kusini
2. Niger
3. Mali
4. Chad
5. Jamhuri ya Afrika ya Kati
6. Djibouti
7. Burkina Faso
8. Ethiopia
9. Senegal
10. Sudan