Nchi 10 za Afrika zinazoongoza kutembelewa na watalii mwaka 2024

0
116

Ripoti ya Maendeleo ya Usafiri na Utalii mwaka 2024, inaonyesha kwamba Afrika Kusini inashikilia nafasi ya juu zaidi barani Afrika, ikifuatiwa na Mauritius na Ghana katika sekta ya Usafiri na Utalii ambapo imechochea uundaji wa ajira na maendeleo ya kiuchumi.

Sekta ya Usafiri na Utalii imechochea uundaji wa ajira na maendeleo ya kiuchumi ambapo pia inatarajiwa kurejea katika viwango vyake vya kabla ya janga la UVIKO-19 mwaka 2024.

Mwaka 2024, Afrika imekuwa na alama ya juu zaidi katika sekta ya usafiri na utalii, ambapo imezalisha kwa wastani wa zaidi ya asilimia 21 ya ajira na asilimia 43 ya wafanyakazi wa sekta hiyo wameajiriwa katika sehemu ambazo zinachukuliwa kuwa na mshahara wa juu zaidi.

Kwa upande wa Tanzania Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania iliyotolewa hivi karibuni imeonesha kwa Machi na Aprili mwaka huu watalii wa kimataifa wameongezeka kwa asilimia 21.9 na 21.8 ikilinganishwa na miezi kama hiyo mwaka jana, hali inayoonesha kuendelea kuimarika kwa sekta ya utalii nchini na duniani.

Hizi ni nchi 10 za Afrika zinazoongoza kutembelewa na idadi kubwa ya watalii kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Usafiri na Utalii mwaka 2024;

  1. Afrika Kusini
  2. Mauritius
  3. Botswana
  4. Kenya
  5. Tanzania
  6. Rwanda
  7. Namibia
  8. Zambia
  9. Ghana
  10. Senegal
Send this to a friend