Gharama ya maisha inaathiri moja kwa moja ustawi wa watu binafsi na jamii kwa ujumla. Hii ni kipimo cha bei ya bidhaa na huduma muhimu kama vile makazi, chakula, usafiri, huduma za afya, na elimu.
Kwa nchi nyingi za Afrika, kupanda kwa gharama hizi kumeibua changamoto kubwa kwa wananchi, hasa wale wa kipato cha chini na cha kati.
Ikilinganishwa na takwimu za kipindi kama hiki mwaka uliopita, Ethiopia sasa inashikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ikiwa na kiashiria cha gharama kubwa za maisha, ikilinganishwa na cha Msumbiji ambayo imeshuka kwa kiasi kikubwa.
Haya ni mataifa ya Afrika yenye gharama kubwa zaidi ya maisha mwanzoni mwa mwaka 2025, kulingana na takwimu za Numbeo.
- Ethiopia
- Botswana
- Msumbiji
- Ivory Coast
- Somalia
- Cameroon
- Mauritius
- Zimbabwe
- Rwanda
- Zambia
Chanzo: Business Insider Afrika