Nchi 10 za Afrika zinazoongoza kwa uhalifu mwaka 2024

0
71

Barani Afrika, uhalifu ni changamoto inayozidi kuongezeka na kuathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Uhalifu una madhara makubwa kuanzia kuvuruga amani na utulivu wa jamii hadi kuzuia maendeleo ya kiuchumi.

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Numbeo, Afrika Kusini inashikilia nafasi ya juu zaidi katika viwango vya uhalifu barani Afrika na kufuatiwa na nchi ya Nigeria.

Miji kama Johannesburg na Cape Town imeorodheshwa kuwa na viwango vya juu vya uhalifu, ikiwa na matukio ya wizi, mauaji, na wizi wa magari.

Hali hii imetokana na sababu mbalimbali zikiwemo umaskini, ukosefu wa ajira, na ukosefu wa usawa wa kiuchumi zinazotengeza mazingira ambapo watu wanaweza kugeukia shughuli haramu kama njia ya kujikimu.

Hizi ni nchi 10 za Afrika zinazoongoza kwa uhalifu mwaka 2024 kwa mujibu wa Numbeo;

  1. Afrika Kusini
  2. Nigeria
  3. Angola
  4. Somalia
  5. Cameroon
  6. Namibia
  7. Mozambique
  8. Zimbabwe
  9. Ivory Coast
  10. Kenya

Chanzo: Business Insider

Send this to a friend