Nchi 10 zenye gharama kubwa zaidi ya mafuta Afrika

0
30

Licha ya kupanda kwa bei za mafuta nchini Nigeria, nchi hiyo si miongoni mwa zile zilizo na bei ya juu zaidi kwa lita barani Afrika. Na hiyo ni kwa sababu Serikali ya Nigeria inatoa ruzuku kwa bidhaa hiyo.

Kuendelea kupanda kwa gharama ya petroli Kusini mwa Jangwa la Sahara kunahusishwa na mgogoro kati ya Urusi na Ukraine,  na kuna hofu kwamba kadiri mzozo unavyoendelea kuongezeka, gharama ya nishati hiyo huenda ikapanda zaidi Afrika.

Iwapo Marekani au nchi za Umoja wa Ulaya zitaamua kurefusha vikwazo vya kiuchumi vya Urusi vinavyozidi kuongezeka kwa kupiga marufuku mafuta yake, hii bila shaka itaonesha janga kwa sekta ya nishati duniani.

Tayari bei ya mafuta duniani imevuka dola 100 kwa kila pipa ambayo ilirekodiwa mara ya mwisho mwaka 2014. Bidhaa hiyo kwa sasa inauzwa kwa $102.6 kwa pipa, kulingana na bei ya Brent Crude.

Sababu nyingine inayochangia kupanda kwa gharama ya nishati barani Afrika ni ukweli kwamba karibu nchi zote zinazoongoza katika uzalishaji wa mafuta barani Afrika zimeshindwa kukuza uwezo wa kuboresha bidhaa ndani ya nchi.

Hizi ni Nchi 10 za Kiafrika zenye bei ya juu ya petroli kulingana na takwimu ililyotolewa na Global Petrol Prices kwa Machi 2022.

1. Zimbabwe: Lita moja ya petroli inagharimu dola 2.153. Zimbabwe si mzalishaji wa mafuta, ingawa kulikuwa na ripoti zinazokinzana kuhusu ugunduzi wa mafuta ghafi Kaskazini mwa Zimbabwe mwaka wa 2018.

2.Shelisheli: Lita moja ya petroli katika nchi hii inauzwa kwa dola 1.541. Kwa sasa visiwa hivi havizalishi mafuta na gesi yoyote, ingawa baadhi ya kampuni ya kimataifa ya mafuta yanashughulika kutafuta akiba ya mafuta katika maeneo yao.

3.Malawi: Inagharimu dola 1.426 kununua lita moja ya petroli,  nchi hiyo inasemekana kuwa na matarajio makubwa ya kugundua hifadhi ya mafuta ghafi katika upande  Ziwa Tanganyika uliopo nchini humo.

4. Afrika Kusini: Hapa, lita moja ya petroli inagharimu dola 1.413. Mnamo mwaka wa 2019.

5. Uganda: Katika nchi hii ya Afrika Mashariki, lita moja ya petroli inagharimu dola 1.389. Kulingana na  Business Insider Africa inaonyesha kuwa hifadhi ya mafuta ghafi nchini humo kufikia 2021, ilifikia mapipa bilioni 2.5.

6. Mauritius: Nchi hii inashika nafasi ya sita kwa bei kubwa zaidi ya petroli, Dola 1.381 kwa lita. Mauritius kwa sasa haizalishi mafuta, ingawa wataalam wanasema kuna matarajio.

7.Burundi: Katika nchi hii ya Afrika Mashariki, lita moja ya petroli inagharimu dola 1.340. Kulingana na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, nchi hii kwa sasa haina vyanzo vyovyote vya ndani vya mafuta ghafi au gesi asilia.

8.Senegal: Katika nchi hii ya Afrika Magharibi inayozungumza lugha ya Kifaransa, inagharimu dola 1.299 kununua lita moja ya petroli. Nchi iligundua amana za mafuta yasiyosafishwa kati ya 2014 na 2017.

9.Lesotho: Katika nchi hii, inagharimu dola 1.231 kununua lita moja ya petroli. Nchi haina amana yoyote ya mafuta iliyothibitishwa.

10.Rwanda: Hapa, lita moja ya petroli inagharimu dola 1.230 tena nchi hii ya Afrika Mashariki haizalishi mafuta ghafi.

Send this to a friend