Nchi 10 zenye idadi kubwa ya Simba duniani

Simba, anayejulikana mara nyingi kama Mfalme wa Wanyama, ni mnyama anayepatikana kiasili barani Afrika na nchini India. Wanyama hawa wakubwa wana uwezo wa kukimbia, kuruka na kupanda kwa kasi inayofikia maili 46 kwa saa, kutokana na miguu yao ya mbele yenye nguvu na miili yao iliyo imara.
Kwa kawaida, simba dume huishi hadi kufikia umri wa miaka 12, wakati simba jike huweza kuishi hadi miaka 16.
Tanzania, iliyopo Afrika Mashariki, inakadiriwa kuwa na takribani simba 14,500 wa porini, idadi kubwa zaidi duniani. Idadi kubwa ya simba hao hupatikana katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba, ambako wanaishi kwa ulinzi na mazingira yao ya asili.
Afrika Kusini pia ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya simba, ikiwa na takribani simba 3,284, jambo linaloifanya kuwa nchi nyingine muhimu kwa uhifadhi wa wanyama hao wakubwa.
Hizi ni nchi 10 zenye idadi kubwa ya Simba duniani;
1. Tanzania: 14,500
2. Afrika Kusini: 3,284
3. Botswana: 3,063
4. Kenya: 2,515
5. Zambia: 2,349
6. Zimbabwe: 1,362
7. Ethiopia: 1,239
8. Sudan Kusini: 866
9. Namibia: 801
10. Msumbiji: 678
Chanzo: World Population Review








