Nchi 10 zenye viboko wengi zaidi duniani

Viboko ni miongoni mwa wanyama wakubwa na hatari zaidi barani Afrika, wanaoishi zaidi katika mazingira ya maji safi kama mito, maziwa na mabwawa. Ingawa mara nyingi huonekana watulivu wanapokuwa majini, viboko ni wanyama wenye nguvu kubwa na hulinda maeneo yao kwa ukali, hasa wanapohisi kutishiwa.
katika miaka ya karibuni, idadi ya viboko imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo uharibifu wa makazi, migogoro kati ya binadamu na wanyamapori, pamoja na ujangili.
Kutokana na hali hiyo, nchi zenye idadi kubwa ya viboko zimekuwa na nafasi muhimu katika juhudi za uhifadhi wa wanyama hawa adimu, huku zikibeba wajibu mkubwa wa kulinda urithi wa asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Hizi ni nchi 10 zenye idadi kubwa ya viboko duniani;
1. Zambia: 37,100
2. Tanzania: 20,000
3. Msumbiji: 20,000
4. Uganda: 10,000
5. South Africa: 7,000
6. Kenya: 6,500
7. Zimbabwe: 5,000
8. Namibia: 3,300
9. Malawi: 3,000
10. Sudan ya Kusini: 2,500
Chanzo: World Population Review








