Nchi 10 zinazoongoza kwa talaka duniani

0
35

Talaka ni ruhusa ya kisheria ambayo mume au mke hupewa wakati anapomuacha mwenzie. Mahakama hufikia uamuzi wa kutoa talaka baada ya kuridhika kuwa ndoa imevunjika kiasi ambacho haiwezi kurekebishika tena.

Kwa mujibu wa watafiti mbalimbali duniani, sababu mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kifedha, kudanganya, kunyimwa unyumba, uraibu n.k huchangia wanandoa kudai talaka katika mataifa mbalimbali.

Hizi ni nchi 10 ambazo wanandoa hupeana talaka zaidi ulimwenguni;

1: Maldives
Kwa upande wa idadi ya talaka katika nchi hii kwa 2023, iko katika nafasi ya kwanza duniani ambapo kuna talaka 5.5 kwa kila watu 1,000.

2. Kisiwa cha Guam
Kisiwa hiki kinashika nafasi ya pili kwa talaka nyingi kikiwa na wastani wa talaka wa asilimia 4.3 kwa kila watu elfu moja.

3: Urusi
Urusi inashika nafasi ya tatu kwa talaka nyingi duniani. Moja ya mataifa makubwa na yenye idadi kubwa ya watu ambapo ina wastani wa asilimia 3.9 ya takala kwa kila watu 1,000.

Nchi 10 za Afrika ambazo watu wake wana furaha zaidi

4. Moldova
Moldova ni moja ya nchi ndogo Mashariki mwa Ulaya ambapo zamani ilikuwa chini ya Umoja wa Soviet. Ina watu milioni 2.6 ikishika nafasi ya nne kwa asilimia 3.8 ya wastani wa talaka.

5: Belarus
Kwa mujibu wa takwimu inashika nafasi ya tano ikiwa na wastani wa asilimia 3.7 ya talaka kwa kila watu 1,000.

6: China
Taifa lenye watu wengi wapatao 1.4 bilioni, pia linakumbana na mizozo ya talaka. Kwa mujibu wa takwimu, ina wastani wa asilimia 3.2 ya talaka.

7: Aruba
Aruba, ni nchi inayounda Ufalme wa Uholanzi iliyoko Kusini mwa Bahari ya Caribbean. Inashika nafasi ya saba kwa talaka, ikiwa na silimia 2.9 katika kila watu 1,000.

8. Georgia
Georgia ina watu milioni 3.7, inashika nafasi ya nane duniani kwa wastani wa asilimia 2.9 ya talaka katika kila watu 1,000.

9. Ukraine
Ukraine yenye watu milioni 43 inapitia kipindi kigumu cha vita dhidi ya Urusi. Inashika nafasi ya 9 kwa utoaji talaka duniani.

10. Costa Rica
Costa Rica ni taifa linalozungukwa na milima, misitu na bahari huko Amerika. Ina watu milioni 5.1, inashika nafasi ya 10 kwa viwango vya talaka duniani ikiwa na wastani wa asilimia 2.8 ya talaka kwa kila watu 1,000.

Send this to a friend