Nchi 15 kutuma waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

0
38

Nchi 15 kupitia Balozi zao hapa nchini zimeruhusiwa kuleta waangalizi wa Kimataifa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba, 2020 baada ya Balozi hizo kuwasilisha maombi na kufuata taratibu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Manfred Fanti, Balozi wa Italia hapa nchini, Roberto Mengoni na baadae Balozi wa Poland, Krzysztof Buzalski

Kabudi ameongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu kwa mara ya kwanza umekuwa tofauti na miaka iliyopita kwa kuwa unafanyika kwa kugharamiwa na fedha za ndani badala ya wahisani jambo ambalo baadhi ya watu walianza kuhofia kutokuwepo kwa waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi.

“Huu ni uchaguzi mkuu ambao kwa mara ya kwanza kwa asilimia 100 tunaugharamia sisi wenyewe kama Serikali ya Tanzania, utaratibu wa uchaguzi chini ya sheria ya uchaguzi na chini ya utaratibu wa Kimataifa huwa tunakuwa na waangalizi wa uchaguzi na mwaka huu nchi hizo 15 kupitia balozi zao zimepata  kibali mara baada ya kufuata taratibu za kuomba kuleta waangalizi wa uchaguzi mkuu,” Amesema Prof. Kabudi.

Waziri huyo amesema kila mgeni/muangalizi atakayefika nchini atatakiwa kuwa na cheti kinachothibitisha kuwa amepimwa na hana maambukizi ya virusi vya corona.

Send this to a friend