Nchi 20 zinazoongoza kwa rushwa Afrika

0
66

Shirika la Transparency International (CPI) linalopambana na rushwa duniani limetoa ripoti yake ya kila mwaka ya rushwa. Nakala ya ripoti hiyo imeonyesha asilimia 90 ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti zilipata chini ya 50, 44 kati ya nchi hizo zilizo na alama za chini sana ni kutoka barani Afrika ambayo inaashiria hali mbaya zaidi ya rushwa.

Katika Bara la Afrika, rushwa imetajwa kuchochewa na mambo kadhaa kama ubabe, ukosefu wa utulivu wa kisiasa/kitaasisi na aina mbalimbali za changamoto zinazosababishwa na migogoro.

Ripoti ya karibuni ya CPI imeonesha wastani wa alama barani Afrika ni 33 ambayo ni ya chini kabisa duniani.

Hii ni orodha ya nchi 20 zinazoongoza kwa rushwa Afrika kulingana na viwango vya hivi karibuni:

Sudan Kusini: Alama 11, ya chini zaidi duniani
Somalia: Alama 13
Libya: Alama 17
Equatorial Guinea: Alama 17
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo: Alama 19
Burundi: Alama 19
Chad: Alama 20
Sudan: Alama 20
Comoro: Alama 20
Guinea Bissau: Alama 21
Congo: Alama 21
Eritrea: Alama 22
Zimbabwe: Alama 23
Nigeria: Alama 24
Jamhuri ya Afrika ya Kati: Alama 24
Guinea: Alama 25
Msumbiji: Alama 26
Madagascar: Alama 26
Uganda: Alama 27
Cameroon: Alama 27

Ripoti ya Transparency International ya mwaka 2019, Tanzania ilipata alama 37 na kushika nafasi ya 96 kati ya nchi 180.