Nchi 5 ambazo hazina maambukizi ya corona hadi leo

0
41

Ikiwa ni takribani miaka miwili sasa dunia ikiendelea kutumia kila mbinu kupambana na Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO19), ni vigumu sana kuamini kwamba kwa kipindi chote hicho kuna nchi ambayo haina au haijaripoti kabisa kisa cha maambukizi.

Hadi sasa zipo nchini tano duniani ambazo hazijaripoti kisa chochote cha maambukizi ya UVIKO19 kwa maelezo kuwa hakuna mtu aliyebainika kuwa na ugonjwa huo. Lakini taarifa za baadhi ya asasi na wanasiasa wa upinzani kwenye nchi hizo zinaeleza kuwa kumekuwepo maambukizi.

Nchi ambazo hazijaripoti kisa chochote ni:

  1. North Korea 🇰🇵
  2. Turkmenistan 🇹🇲
  3. Tonga 🇹🇴
  4. Tuvalu 🇹🇻
  5. Nauru 🇳🇷

Rais wa Turkmenistan ambaye ameongoza taifa hilo tangu mwaka 2006 ametupilia mbali taarifa za uwepo corona kwenye nchi yake na kuueleza Umoja wa Mataifa kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa huo yasigeuzwe kuwa siasa.

Hadi Juni mwaka huu, Korea Kaskazini ililieleza Shirika la Afya Duniani kuwa limewapima zaidi ya watu 30,000 lakini halijabaini uwepo wa virusi hivyo kwa mtu yeyote.

Zaidi ya visa milioni 219 vimeripotiwa hadi sasa duniani kote, huku kati ya hivyo watu zaidi ya milioni 4.6 wakifariki dunia.

Send this to a friend