Nchi 5 za Afrika zenye mifumo bora zaidi ya elimu

0
65

Elimu ndiyo silaha yenye nguvu zaidi ambayo unaweza kuitumia kubadilisha ulimwengu, wakati huo huo inasaidia watu kuwa raia bora, kupata kazi yenye malipo bora na kuonesha tofauti kati ya mema na mabaya.

Hizi ni Nchi 5 zenye mifumo bora zaidi ya elimu Afrika kwa mujibu wa NewsNowGh
1. Shelisheli
Hii ni nchi ya visiwa inayotambuliwa kama nchi pekee ya Kiafrika ambayo imefikia elimu ya UNESCO (Shirika la umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni) kwa malengo yote. Nchi hii elimu bila malipo ni ya lazima kwa watoto hadi umri wa miaka 18, wanafunzi wanatakiwa kununua sare za shule pekee. Shelisheli imepewa alama 69.3, kwa upande wa elimu na kongamano la elimu duniani.

2. Africa Kusini
Nchini Afrika Kusini, elimu ya msingi iko katika awamu tatu na hudumu kwa miaka sita. Elimu bila malipo ni ya lazima kwa watoto kuanzia umri wa miaka 6 hadi 15. Serikali ya Afrika Kusini inatoa michango mikubwa kwa ukuaji wa mfumo wa elimu nchini humo, kwani 18% ya matumizi ya taifa yanatumika kwa elimu. Umuhimu mkubwa ambao Serikali iliweka kwenye elimu umefanya vyuo vikuu vya Afrika Kusini kuwa vya juu barani Afrika na ulimwenguni.

3. Mauritius
Nchi inaendesha mfumo rasmi wa elimu wa 3-6-5-2. Serikali ya Mauritius inatoa elimu ya bure kwa raia wake kuanzia ngazi ya awali hadi ya elimu ya juu. Hata hivyo, elimu ni ya lazima kwa kila raia hadi umri wa miaka 16. Kadhalika, shule zote zinazomilikiwa na Serikali zinamiliki angalau kompyuta kumi. Wanafunzi wa shule za msingi hupata vitabu vya bure, zaidi ya hayo, serikali ilianzisha usafiri wa bure kwa wasomi wote.

4. Tunisia
Serikali ya Tunisia imefanya elimu kuwa ya lazima na bure kwa raia wake wote kuanzia ngazi ya msingi hadi elimu ya juu. Mfumo wa elimu nchini Tunisia umeundwa katika viwango vya msingi, vya kati, vya Sekondari, vya ufundi stadi na vya elimu ya juu.

Serikali ya Tunisia iko katika ushirikiano endelevu na wafadhili na mashirika ya kimataifa katika jitihada za kusaidia maendeleo ya elimu nchini humo. Zaidi ya hayo, serikali na watu binafsi wametoa michango mikubwa kwa maendeleo ya mfumo wa elimu nchini Tunisia.

5. Kenya
Jamhuri ya Kenya inaendesha mfumo rasmi wa elimu wa 8-4-4. Nchini Kenya, elimu ya msingi na sekondari ni bure lakini si ya lazima. Viwango tofauti vya elimu nchini Kenya vinajumuisha elimu ya msingi, sekondari, ufundi, na elimu ya juu. Sera ya serikali ya Kenya inabainisha muda wa miaka 8 ya elimu ya lazima kwa raia wake.